Picha 10: MKAPA ALIVYOKABIDHI JENGO LA UPASUAJI SIMIYU.

Rais Mstaafu awamu ya tatu Benjamini Mkapa, akisalimia na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Titus Kamani, baada ya kuwasili Mkoani humo katika kijiji cha Nkoma wilaya ya Itilima, kwa ajili ya kuzindua jengo la upasuaji katika kituo cha Afya Nkoma jengo hilo limejengwa na Taasisi ya Mkapa Faundation kwa shilingi Milioni 270.


Rais Mstaafu awamu ya tatu Benjamini Mkapa akikata utepe kuashiria kuzinduliwa kwa jengo la upasuaji katika kituo cha Afya Nkoma, kilichopo wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu. (wa kwaza kulia) Balozi wa Japan Nchini Masaharu Yoshida. (Kushoto) Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Ummy Mwaimu jengo hilo limejengwa na Taasisi ya Mkapa Faundation kwa shilingi Milioni 270.

Rais Mstaafu awamu ya tatu Benjamini Mkapa akisoma bango baada ya kuzindua jengo la upasuaji katika kituo cha Afya Nkoma, kilichopo wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu. (kushoto) Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Mkapa Faundation Dk Ellen Senkoro jengo hilo limejengwa na Taasisi ya Mkapa Faundation kwa shilingi Milioni 270.


Rais Mstaafu awamu ya tatu Benjamini Mkapa akikagua moja ya vifaa vya kutibu wagonjwa vikiwemo vitanda, katika kituo cha Afya Nkoma, alipowasili katika kituo hicho kwa ajili ya kuzindua Jengo la Upasuaji kwa kituo hicho, jengo hilo limejengwa na Taasisi ya Mkapa Faundation kwa shilingi Milioni 270.Rais Mstaafu awamu ya tatu Benjamini Mkapa, pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka, wakiwasalimia wananchi wa kijiji cha Nkoma wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu, baada ya kuwasili kwa ajili ya kuzindua Jengo la Upasuaji katika kituo cha Afya Nkoma jengo hilo limejengwa na Taasisi ya Mkapa Faundation kwa shilingi Milioni 270.


Rais Mstaafu awamu ya tatu Benjamini Mkapa, pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka, wakiwasalimia wananchi wa kijiji cha Nkoma wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu, baada ya kuwasili kwa ajili ya kuzindua Jengo la Upasuaji katika kituo cha Afya Nkoma jengo hilo limejengwa na Taasisi ya Mkapa Faundation kwa shilingi Milioni 270.

Waziri wa AFya Maendeleoya Jamii, Jinsia,Wazee, na watoto Ummy Mwalimu akiongea na wananchi kijiji cha Nkoma leo Wilayani Itilima Mkoa wa Simiyu, wakati wa hafla ya kuzindua jengo la upasuaji katika kituo cha Afya Nkoma, kilichojengwa na taasisi ya Mkapa faundation,


Mbunge wa Jimbo la Itilima Njalu Silinga (wa kwaza kushoto) Waziri wa AFya Maendeleoya Jamii, Jinsia,Wazee, na watoto Ummy Mwalimu, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka, Mbunge wa Busega Rafael Chegeni, wakicheza Ngoma ya kisukuma wakati wa hafla ya kuzindua jengo la upasuaji katika kituo cha Afya Nkoma, kilichojengwa na taasisi ya Mkapa faundation.

Rais Mstaafu awamu ya tatu Benjamini Mkapa akimkabidhi cheti cha ushirikiano mzuri, Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Itilima Daud Nyalamu, wakati wa hafla ya kuzindua jengo la upasuaji katika kituo cha Afya Nkoma, kilichojengwa na taasisi ya Mkapa faundation.

 RAIS mstaafu wa Awamu ya tatu Benjamin mkapa Leo amezindua na kukabidhi Jengo la Upasuaji katika kituo cha Afya Nkoma kilichopo wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu. 

Jengo hilo ambalo limejengwa na taasisi ya Mkapa Foundation kwa kushirikiana na nchi ya Japan limegharimu milioni 270 ambapo wakinamama wajawazito, watoto na wagonjwa walikuwa wakiipata huduma hiyo umbali wa kilomita 40.

 Mkapa ameishukuru nchi ya Japan ambao walitoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa jengo hilo kupitia taasisi ya Mkapa foundation, huku lengo likiwa kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga.

“ Nchi yetu bado tunakabiliwa na changamoto ya vifo vya akina mama wajawazito pamoja na watoto wachanga, Nchi ya Japan wametoa msaada huo kwa ajili ya kukabiliana na changamoto hii, taasisi ya Mkapa foundation itaendeleza ushirikiano na serikali katika kutatua changamoto mbalimbali za afya” alisema Mkapa.

Mbunge wa Jimbo la Itilima Njalu Silanga alisema kuwa pamoja na kukamilika kwa jengo hilo upungufu wa watumishi bado ni changamoto kubwa wajibu wa serikali ni kuajiri watumishi ili waeze kuhudumia wananchi.

Baadhi ya wananchi waliohudhuria katika ufunguzi huo walisema kuwa jengo hili limeongeza faraja kwa akinamama wajawazito na wagonjwa kwani wengi wao walikuwa wakifia njiani wakati wakisafirishwa kwenda Bariadi kupata huduma ya upasuji.

 
Previous
Next Post »