ILIVYOKUWA UZINDUZI WA (REA) AWAMU YA TATU SIMIYU.

Afisa Mahusiano shirika la Umeme Tanesco Mkoa wa Simiyu Ben Kirumba, akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Nishati na Madini Medard Kalemani matumizi ya kifaa cha U-META (Umeme Tayari), ambacho unaweza kutumia bila ya kufunga waya kwenye nyumba ya vyumba visivyozidi vitatu. Naibu Waziri huyo alikuwa kwenye hafla ya kuzindua Mradi wa Umeme Vijiji (REA) awamu ya tatu katika kijiji cha Nangale wilaya Itilima.

Naibu Waziri Nishati na Madini Medard Kalemani akiwaonyesha wananchi kifaa cha umeme U-META (Umeme Tayari), ambacho unaweza kutumia bila ya kufunga waya kwenye nyumba ya vyumba visivyozidi vitatu, wakati wa hafla ya kuzindua Mradi wa Umeme Vijiji (REA) awamu ya tatu katika kijiji cha Nangale wilaya Itilima.


Habari kubwa leo katika mkoa wa Simiyu, ni kuzinduliwa kwa mradi wa umeme vijiji awamu ya tatu (REA) katika mkoa huo, ambapo Naibu waziri Nishati na Madini Medard Kalemani alikuwa mgeni rasmi akiambata na Mkuu wa mkoa wa Simiyu Antony Mtaka na wabunge wa Mkoa huo.

Hafla hiyo imefanyikia katika kijiji cha Nangale kilichopo wilaya ya Itilima, ambapo jumla ya vijiji 347 ambavyo vilikuwa bado havijapata umeme wakati wa utekelezaji wa mradi huo kwa awamu ya kwanza na pili vinatarajiwa kupatiwa umeme.

Mbali na vijiji hivyo taasisi zote za serikali, nyumba za ibada, misikiti na makanisa vitanufaika na mradi huo ambao utatekelezwa kwa muda wa miezi 24 kwa gharama ya shilingi Bilioni 33.47.

Mkandarasi ametajwa kuwa ni White City International Contractors ambaye atashirikiana na Guangdong Jianneng Electric Power Engineering Co.Ltd.

Naibu waziri huyo amemtaka mkandarasi huyo kufanya kazi kwa bidii na kumaliza ndani ya muda, huku akisema kila nyumba itawekewa umeme.

" Hata nyumba za Tembe awamu hii lazima ziweke umeme, hakuna kijiji, kitongoji, nyumba ambayo italukwa, na mkandarasi hakikisha hakuna kuruka nyumba, kijiji au kitongoji na taasisi za umma" alisema Kalemani.

Wabunge Njalu Silinga (Itilima) Ester Midimu (Viti maalum), Mashimba Ndani (Maswa Magharibi) pamoja na Rea Komonya (Viti maalum) wameomba taasisi zote za serikali kufikishiwa umeme, huku wakiwataka wananchi kunufaika na mradi huo kwa kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo.
Newest
Previous
Next Post »