TAKUKURU SIMIYU WALIVYOSADIA KUREJESHWA MILIONI 80 ZA POSHO, SAFARI HEWA.

Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Simiyu Adili Elinipenda, akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa taasisi hiyo ikitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu yake katika kipidi cha Julai 1, 2016 hadi Machi 30, 2016 Leo hii. (kushoto) ni Mkuu wa dawati la elimu kwa umma Aquilinus Shiduki, (kulia) Ni kaimu Kamanda wa Taasisi hiyo Alex Mpemba.

Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Simiyu Adili Elinipenda, akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake leo wakati wa taasisi hiyo ikitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu yake katika kipidi cha Julai 1, 2016 hadi Machi 30, 2016.

Habari kubwa kutoka katika Mkoa wa Simiyu leo hii, ni Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani humo.

Zilikuwa shilingi Milioni 80,252,916, na senti 46 kiasi ambacho kinaelezwa kuwa ni pesa ya Umma ambayo ilikuwa imetumika katika Semina hewa, Posho zisizostahili, Manunuzi hewa, mishahara hewa kwa watumishi wa umma hasa idara ya elimu.

Pesa hizo zinaelezwa kuwa zimetumika bila ya kufuata sheria, Kanuni na taratibu, hivyo taasisi hiyo imefanikiwa kuziokoa pesa hizo, ambapo wahusika wamezirejesha na nyingine zimeokolewa zisitumike isivyokuwa.

Mchanganuo wa pesa hizo ni kama ifuatavyo, Safari hewa Milioni 25,132,447.96, Manunuzi hewa 13,374,000.00, mishara hewa idara ya elimu 40,346,468.50 pamoja na posho zisizostahili ni Milioni 1,400,000.

Kati ya watu walirejesha fedha hizo ni Baadhi ya madiwani katika halmashauri ya mji wa Bariadi, ambao wanadaiwa kujilipa posho kinyume cha utaratibu.

Hata hivyo taasisi hiyo kwa kipindi hicho imepokea taarifa za vitendo vya rushwa jumla 75 huku Mabaraza ya ardhi, Mahakama vikiwa vyombo vya kutoa haki zilivyoko chini ya serikali vikiongoza kwa kutolewa taarifa 15 za vitendo hivyo.

Idara nyingine ya serikali ni Jeshi la polisi ambalo ndilo linafuatia kwa taarifa za vitendo vya rushwa jumla zikiwa 12 zilizopelekwa Takukuru, ikifuatiwa idara ya afya, elimu, ardhi.

Taasisi hiyo imewaomba wadau wote na wananchi kwa ujumla kupiga vita vitendo vya rushwa ikiwa pamoja na kutoa taarifa haraka ikiwa watagundua kuwepo kwa vitendo hivyo sehemu yeyote, huku ikiomba ushirikiano kwa watu wanaotakiwa kutoa ushahidi kwenye kesi zinazoendeshwa na taasisi hiyo.

Previous
Next Post »