PICHA 13: KILICHOJIRI MKUTANO MKUU CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI SIMIYU.

Wajumbe wa Mkutano Mkuu Chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Simiyu (SMPC) wakifuatilia kwa karibu mada mbalimbali na ajenda za mkutano mkuu uliofanyika jana Mjini Bariadi katika ukumbi wa ofisi za chama hicho. Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habarI Mkoa wa Simiyu (mwenye shati la njano) akiwa na Katibu Msaidizi wa Klabu hiyo Costantine Mathias wakimkaribisha Kamishena Msaidizi wa jeshi la polisi Mkoani Simiyu Beneventura Mushongi pamoja na Mkuu wa upelelezi mkoa Jonathan Shana (mwenye koti) walipowasili katika ofisi za chama hicho mjini Bariadi jana wakati kikao cha mkutano mkuu wa wanachama wa klabu hiyo.


Mwenyekiti wa muda Faustine Fabian ambaye ni Mwandishi wa habari Kampuni ya Mwananchi, akiongoza kikao.


Viongozi wa Klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Simiyu (SMPC) wakiwa katika picha ya pamoja na Kamishena Msaidizi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu Boniventura Mushongi pamoja na Mkuu wa upelelezi wa jeshi hilo Mkoa Jonathan Shana mara baada ya Kamishena huyo kufungua Mkutano Mkuu wa klabu hiyo uliofanyikia katika ukumbi wa ofisi hizo mjini Bariadi.

Mmoja wa Wajumbe akichangia mada, ambaye ni Mwandishi wa habari wa Gazeti la Nipashe. Shushu Joel.


Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Simiyu Frank Kasamwa akitoa taarifa ya maandeleo ya klabu hiyo Mbele ya Kamishena Msaidizi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu Boniventura Mushongi wakati wa Mkutano Mkuu wa wanachama wa klabu hiyo uliofanyikia katika ukumbi wa ofisi ya klabu mjini Bariadi. ambapo kiongozi huyo alikuwa mgeni rasmi katika mkutano huo.

Kikao kikiendelea.

Picha ya pamoja Viongozi wa Klabu pamoja na Mgeni rasmi.Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Simiyu Frank Kasamwa akiendelea na Kikao cha Mkutano Mkuu wa klabu hiyo.

Mkuu wa upelelezi Mkoa wa Simyu Jonathan Shana akiongea wakati wa kikao hicho.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao.


Na COSTANTINE MATHIAS, SIMIYU.

WAANDISHI wa habari nchini wametakiwa kusimamia maadili ya taaluma yao kwa ni kuwa nguzo ya maendeleo kati ya serikali, wananchi  na wadau mbalimbali katika ufanisi wa shughuli za kila siku.

Hayo yalibainishwa jana na Kamanda wa Polisi mkoa wa Simiyu Bonaventure Mshongi wakati akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa Waandishi wa Habri mkoa wa simiyu uliofanyika katika ofisi za wanahabari mkoani hapo.

Kamanda Mshongi alisema kuwa uandishi wa habari ni nguzo ya maendeleo kwa kwa kuwa unahamasisha serikali, wadau mbalimbali na wananchi kujituma pia uandishi wa habari ni radi ambayo ikitua popote lazima kuacha alama aidha kwa kuonya au kusifu.

‘’jeshi la polisi linawategemea sana waandishi wa Habari katika kufichua maovu kwa umma…lisaidieni jeshi katika kutoa elimu ya ulinzi na usalama kupitia taaluma yenu kwani bila wanahabari sisi hatuwezi kupata taarifa zozote kama mnazopata ninyi’’alisema Mshongi.

Aliwataka wanahabari kutoa ushirikiano katika kujenga mkoa wa Simiyu kwa kuwa karibu na wananchi hasa katika kuwasemea shida zao kwa serikali, huku akisisitiza waandishi kuwa na umoja ili kufanya kazi kwa weledi pia kuweza kuonyana wao wenyewe pindi wanapokiuka maadili ya taaluma yao.

Aliongeza kuwa waandishi wa habari wanatakiwa kuonyesha umoja, kusaidiana pindi wanapopatwa na madhirana klabu iwe na nguvu kuliko mtu mmojammoja.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi na kusoma taarifa maendeleo ya klabu hiyo Mwenyekiti wa Wanahabari mkoa wa Simiyu Frank Kasamwa alisema kuwa hadi sasa klabu imejenga mahusiano na wananchi na taasisi za umma na watu binafsi.

Alisema kuwa hadi sasa klabu inakamilisha mpango wa kuanzisha duka la kuuza vifaa vya maofisini kama mradi wa kuendesha klabu ili kuondokana na utegemezi wa wahisani na wadau.

Aliongeza kuwa wandishi wa habari mkaoni hapa wameweza kutembelea maeneo mbalimbali kwa ajili ya mafunzo kama vile kigoma, Shinyanga, Maswa, Mwanza, Meatu na Butiama ili kuwaongezea weledi wa kazi zao za kila siku.

‘’katika shughuli za kijamii tumeweza kutoa misaada kwa kutembelea kituo cha watoto yatima cha K.K.K.T mjini Bariadi, wadau wametumia klabu kupata huduma ya habari kama vile matangazo ya kupotelewa na kuomba msaada wa matibabu’’ alisema Kasamwa.

Aliongeza kuwa Klabu hiyo inakabiliwa na ukosefu wa fedha kwa ajili ya ukusanyaji wa kazi za waandishi ili kuzitunza kama kumbukumbu, ukosefu wa fedha za chumba cha biashara na fedha za kununulia mashine ya kielektroniki (EFD machine).

Previous
Next Post »